HISTORIA FUPI YA CHUO CHA UALIMU TANGA ELITE
Chuo cha ualimu Tanga Elite ni taasisi binafsi inayotoa mafunzo ya ualimu katika ngazi mbalimbali za kielimu ili kuweza kuisaidia serikali kupambana na wimbi la uhaba wa waalimu nchini
USAJILI.
Chuo cha ualimu Tanga elite kimethibitishwa na kupewa usajili wa serikali kupitia Baraza la usimamizi vyuo vya ufundi nchini NACTE,
Usajili namba REG.NO.(NACTE;REG/TLF/128)
KAULI MBIU
‘Ualimu ni wito,Mwalimu bora Mazingira bora ya utendaji kazi’
MAFUNZO YA VITENDO
Mwanachuo wa Tanga Elite awapo chuoni anapata nafasi ya kujifunza kwa nadharia na vitendo kuhusu mafunzo yote ya ualimu pamoja na chuo kumsaidia kupata shule mbalimbali za kwenda kufanya mazoezi kwa vitendo (BLOCK TEACHING PRACTICE, BTP)
WAKUFUNZI NA WAFANYAKAZI
Chuo kina wafanyakazi na wakufunzi wa kutoshana wenye uzoefu kuhudumia wanachuo wawapo chuoni
MIUNDOMBINU
Chuo cha ualimu Tanga Elite kina miundombinu mizuri ya kuhudumia wanachuo wote kama vile.
• Madarasa ya kutosha
• Chumba cha kompyuta
• Hosteli na vitanda vya kutosha
• Viwanja vya michezo
• Bwalo la chakula
WAHITIMU
Wakati wa kuhitimu mafunzo ya Ualimu katika madaraja mbalimbali chuo kinafanya mahafali ya kuwaaaga wahitimu wote pamoja na kutunukiwa vyeti na zawadi mbalimbali kwa wahitimu waliofanya vizuri.
CHUO KILIPO
Chuo kipo mkoa wa Tanga,katika mji mdogo wa Pongwe,kilometa tatu kutoka barabara ya lami(3km) eneo la mizani.Kwa mawasiliano zaidi tafadhali wasiliana na Mkuu wa chuo kwa namba